WAZIRI JAFO- SERIKALI INAKUZA UWEKEZAJI KUCHOCHEA UCHUMI
Na MWANDISHI WETU
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Seleman Jafo, amesema serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka fursa mbalimbali za uwekezaji nchini kuhakikisha wafanyabiashara wanakuza uchumi wao na Taifa.
Pia, ametoa maagizo kwa watumishi wa Wizara hiyo na Tume ya Ushindani (FCC), kuhakikisha wanashughulikia changamoto zilizopo za uwekezaji huku akiitaka FCC kuharakisha miungano sahihi ya Taasisi za kibiashara kukuza uchumi.
Jafo ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati akifungua maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ushindani Duniani, yaliyoandaliwa Kitaifa na Tume ya Ushindani (FCC).
"Serikali ya Rais Dk.Samia imeendelea kufanya maboresho mbalimbali ya Taasisi ikiwemo ya uwekezaji (TIC) kwa lengo la kukuza uwekezaji nchini.
"Kama hiyo haitoshi, katika kuboresha mazingira ya biashara nchini Rais Dk.Samia ameunda tume ya maboresho ya kodi, kuhakikisha zinashamiri na kufanyika kwa wepesi zaidi," amesema.
Reviewed by Gude Media
on
December 05, 2024
Rating:
