Katibu Jessica ataka vijana wasitumike kisiasa kuvuruga amani na uchaguzi
Na MWANDISHI WETU
KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Taifa, Jessica Mashama, amewataka vijana wote nchini kujitokeza kwa wingi katika kuboresha taarifa zao za daftari la wapiga kura linalotarajiwa kuanza Mei Mosi hadi saba, mikoa mbalimbali, kupata sifa ya kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka akiwemo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Pia, amewataka vijana kuwaepuka viongozi wanaotaka kuwatumia kisiasa kuvuruga amani, bali waitunze kuepuka wale wote wenye nia ovu hususan kipindi hiki cha uchaguzi kwani usalama ndiyo msingi mkubwa wa maendeleo.
"Ni haki ya msingi ya kila kijana kujitokeza kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka, hivyo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume huru ya Uchaguzi uhakiki huo utafanyika kuanzia Mei Mosi hadi 7 katika mikoa 15, vijana wajitokeze kwa wingi," amesema.
Ametaja baadhi ya mikoa hiyo ni Geita, Kagera, Mara, Simiyu, Mwanza Kigoma, Iringa, Ruvuma, Mbeya.
Amesema vijana wamejipanga vyema kushiriki uchaguzi, wako tayari kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka hususan wale wanaotokana na CCM na kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali.
Amesema vijana wako tayari kwa uchaguzi na kuwachagua viongozi bora akiwemo mgombea wa CCM, Rais Dk.Samia na Mgombea mwenza wake, Dk.Emmanuel Nchimbi, kwani amefanya mambo makubwa nchini hususan sekta ya elimu kwa kujenga shule nyingi msingi na sekondari, vyumba vya kutosha vya madarasa, miradi ya kimkakati SGR na Bwawa la Mwalimu Nyerere.
Ametaja miradi mingine, aliyoitekeleza Rais Dk.Samia ni kuimarisha miradi ya maji vijijini na mjini, miundombinu, na kuimarisha maridhiano, amani nchini, jambo ambalo limekuwa na tija kubwa ya kuchochea maendeleo.
Reviewed by Gude Media
on
April 30, 2025
Rating:
