Mkurugenzi Igunga, Selwa awataka wananchi kutumia fursa madaktari bingwa wa Rais DK. Samia kupata huduma za afya
IGUNGA TABORA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora, Selwa Hamid, ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa ya kuwepo Madaktari Bingwa walioanza kutoa huduma katika Hospitali ya Wilaya kwa lengo la kupata ufumbuzi wa maradhi yanayodaiwa kuwakabili.
Selwa ametoa wito huo baada ya kuwapokea Madaktari Bingwa wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wanaopiga kambi ya siku tano katika Hospitali hiyo mjini hapa.
‘’Wenye changamoto ya maradhi mbalimbali niwaombe mjitokeze kwa wingi mpate tiba na kuona neema ya Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetufikia Igunga,’’ametoa wito.
Aidha, amesema maradhi sugu yatakua yamepata matibabu, hivyo wanapoondoka Madaktari Bingwa hao na maradhi yawe yameondoka na kuwaacha wananchi wa Igunga wakiwa salama na afya.
Reviewed by Gude Media
on
April 28, 2025
Rating:



