Mkuu wa Wilaya ya Igunga Sauda kuwachukulia hatua watakaofanya udanganyifu katika zao la pamba
Na MWANDISHI WETU, SHINYANGA
Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora, Sauda Mtondoo, ametoa tahadhari na kuahidi kuwachukulia hatua watakaoweka mchanga laini, maji na vikonyo katika pamba, msimu huu unaotarajiwa kuanza wiki ya kwanza Mei, mwaka huu.
Sauda ameyasema hayo, jana, mkoani Shinyanga alipokuwa katika ziara na viongozi wa Kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira kutembelea viwanda vya kuchakata pamba mkoani humo, kufuatia madai ya uwepo wa uchafu katika zao hilo.
"Hakika tumejionea uhalisia, hasara hii tunaiona siyo tu kwa kampuni hata kwa upande wa serikali kwa sababu mbegu inayoharibika inatarajiwa iende katika mzunguko, halafu irudi katika uzalishaji, hivyo ikikataliwa maana yake ni kuondoa mbegu katika mzunguko wa mbegu bora kwa wakulima wetu," amesema.
Aidha, Sauda amesema wanayo kazi kubwa yakufanya hususan kukabiliana na viongozi wa AMCOS kwa kuwataka kuendelea kuwa waadilifu na kuwasimamia wakulima wa pamba kwa lengo la kuhakikisha madai hayo hayajitokezi tena.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya, Sauda ameambatana na Mwenyekiti na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Igunga, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na Wakuu wa Idara na Vitengo na kutembelea kiwanda cha Fresho investment, Afrisian Ginning na Gaki investment.
Mkuu wa Wilaya ya Igunga Sauda kuwachukulia hatua watakaofanya udanganyifu katika zao la pamba
Reviewed by Gude Media
on
April 17, 2025
Rating:
Reviewed by Gude Media
on
April 17, 2025
Rating:


.jpg)


