Mtevu: Wanaosumbua madiwani katika kata waorodheshwe majina
Wananchi Kigamboni wanasema hawana deni na Rais Dk. Samia kwa mambo mazuri makubwa aliyofanya katika kata hiyo
MWANDISHI WETU
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtevu, amekemea tabia mbaya ya watu wanaowasumbua wanaowasumbua madiwani kutekeleza majukumu yao.
Mtemvu alitoa wito, katika kufunga semina ya mafunzo kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Kata ya Kigamboni na kuwasilisha utekelezaji wa Ilani ya CCM, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Amesema CCM wanautaratibu wao wa kuwapata viongozi na unaeleweka muda wa kuchukua fomu ukifika Chama na serikali itatoa taarifa, ni makosa makubwa kuwaingilia madiwani katika utendaji wa kazi zao.
"Nawataka wenyeviti wa kata kuorozesha majina ya watu ambao wameanza kuwafanyia fujo madiwani wasitekeleze majukumu yao, siyo tabia nzuri na siyo utaratibu wa Chama, wasubiri hadi Chama na serikali itakapotoa taarifa kama ilivyo kwa utarabu wetu", amesema.
Pia, Mtemvu amewata wajumbe hao wasifanye makosa ifikapo Oktoba katika uchaguzi mkuu kwa kuendelea kuichagua CCM.
Amesema Mkoa wa Dar es Salaam, una kura milioni 4, kwa kazi aliyoifanya Rais Dk. Samia wana uhakika wakupata kura zaidi ya milioni 3.5 wakijipanga vizuri.
"Msifanye makosa katika uchaguzi mkuu, pia waacheni wapinzani waendelee kupiga mayoe na nyiniyi msirudi nyuma, kwani wapinza ni waoga ndiyo maana hawataki uchaguzi, watambua kuwa CCM tumejipanga, Rais Dk. Samia amefanya kazi kubwa sana", alisema.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Kigamboni, Datto Msawa, akiwasilisha utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kata hiyo, alisema kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Samia, wananchi hawana deni na Rais Dk. Samia, kutokana mambo mambo makubwa aliyofanya Kigamboni.
Dotto amesema wamenufaika na miradi mingi ikiwemo ujenzi wa barabara mpya za lami, sekta ya afya, maji na elimu.
Amesema katika sekta ya elinu wamepata Shule ya Sekondari ya Ghorofa Paul Makonda, kupitia mradi wa booster, madarasa mapya na ukarabati wa madarasa ya zamani katika shule za msingi zilizopo ndani ya Kata ya Kigamboni.
"Kwa upande wa sekta ya Afya mbali na gari la kubebea wagonjwa, wamepata mashine ya kisasa ya X-ray katika kituo cha Afya Kigamboni, wamejenga jengo jipya la huduma ya mama na mtoto na uboreshaji wa huduma za afya.
Pia, Dotto alisema kata hiyo imenufaika kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu kupata mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri, pia zaidi ya vijana 100 wamepata mafunzo ya ufundi kutoka Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), kupitia jukwaa la uwezeshaji vijana kiuchumi inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Watu Wenye Ulemavu.
Reviewed by Gude Media
on
April 27, 2025
Rating:








