RC Chacha apiga 'jeki' timu ya Igunga United inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Mkoa
Na MWANDISHI WETU, IGUNGA
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha ameipa timu ya Igunga United Sh. milioni 1.5 na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Sauda Mtondoo naye amechangia Sh. 300,000 kusaidia timu hiyo kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Mkoa.
Akizungumza kwa niaba ya Chacha, Sauda amesema mkuu wa mkoa baada ya kupata taarifa ya timu hiyo kushiriki mashindano hayo amefurahi na kueleza anatambua mchango wa timu hiyo.
‘’Ndugu wachezaji, Mkuu wa Mkoa, Paul Matiko Chacha ametoa sh. milioni 1.5 na mimi ninawaongeza Sh. 300,000 katika safari yenu hii, tambueni sisi viongozi wenu tuko nyuma yenu kwa lengo la kuhakikisha ushindi unapatikana,’’ amesema.
Pia Sauda amewakumbusha wachezaji wa timu hiyo, wamebeba dhamana siyo tu ya wilaya hiyo, bali ni ya mkoa, hivyo watakapokuwa uwanjani wakumbuke maneno haya kwa lengo la kuwatia ari ya kupata ushindi dhidi ya timu watakazokabiliana nazo katika mashindano hayo.
Reviewed by Gude Media
on
April 22, 2025
Rating:



