Fanyeni kazi kwa bidii, weledi na kujituma kujenga taifa: DC Mtondoo
IGUNGA TABORA
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Sauda Mtondoo amewakumbusha Wafanyakazi kuwa hakuna haki pasipo wajibu, hivyo wanaowajibu wa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma kwa lengo la kuendelea kulijenga Taifa huku serikali ikiendelea kufanyia kazi haki zao za msingi.
DC. Sauda ameyasema hayo wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani yaliofanyika kimkoa wilayani Nzega mkoani hapa.
‘’Sisi viongozi tunaendelea kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Wafanyakazi katika kulijenga Taifa hili kwa kufanya kazi kwa weledi na umahiri, hivyo shughuli za maendeleo zinakwenda kwa kasi na Taifa linaendelea kusimama imara wakati wote katika sekta ya kijamii, siasa na uchumi,’’ amesema.
Kwa upande wa Mwakilishi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Selwa Hamid aliwasihi wafanyakazi kuendelea kujipongeza kwa sababu ya kazi nzuri wanazofanya.
Reviewed by Gude Media
on
May 01, 2025
Rating:



