Vikundi 27 vya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga vyapatiwa mkopo wa zaidi ya Sh. milioni 300
IGUNGA TABORA.
Vikundi 27 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani vimepewa mkopo wa zaidi ya Sh. milioni 300, zitokanazo na mapato ya asilimia 10 katika halmashauri hiyo.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi hundi ya fedha kwa vikundi vitano vya Wanawake, vikundi 15 vya vijana na Watu wenye Ulemavu saba katika ukumbi wa Maxwel mjini hapa, Mkuu wa Wilaya hiyo, Sauda Mtondoo amewataka kuzingatia nidhamu ya kurejesha walichokopa.
“Kila mmoja anapaswa kuzingatia kurejesha alichokopeshwa kwa sababu katika hili hatutaacha kuwafuatilia kwa kina kwa lengo la kuhakiksha kila senti uliyopaswa kuirejesha unairejesha,’’amesisitiza.
Aidha, DC Sauda amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya dhati yakuona Watanzania wanainuka kutoka katika umasikini sio tu kupitia taasisi za kibenki lakini kupitia mikopo itokanayo na asilimia 10 za mapato ya Halmashauri zote nchini bila kuwa na riba.


