Airtel, UNICEF wakabidhi Vifaa vya Intaneti ya kasi kwa Shule za Sekondari 30 jijini Dodoma
Na MWANDISHI WETU
Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel, kushirikiana na Shirika la Kimataifa la kuhudumia Watoto( UNICEF) wamegawa vifaa vya Intenet yenye kasi kuimarisha elimu ya kidijitali Dodoma.
Kampuni ya Airtel Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi wake wa kijamii wa Airtel SmartWASOMI, wamekabidhi na kufunga vifaa vya intaneti ya kasi kwa shule za sekondari 30 mkoani Dodoma.
Vifaa hivi vitawawezesha walimu na wanafunzi kupata huduma ya intaneti bure, kujisomea kupitia maktaba mtandaoni ya Taasisi ya Elimu Tanzania na majukwaa ya elimu.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Mtemi Mazengo, Mkoani Dodoma, Meneja wa Kanda ya Airtel Tanzania Dodoma, Salum Ngururu alisema, SmartWASOMI siyo tu mtandao, ni mfumo wa kidijitali unaoleta vifaa, maudhui ya kielimu yanayolingana na mtaala na jukwaa la usomaji na ufundishaji wa kisasa.
“Mpango huu unaunga mkono jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano katika kutumia teknolojia ya mawasiliano (TEHAMA) kwenye sekta ya elimu,” alisema meneja huyo.
Naye Grace Samwel akizungumza wa niaba ya Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma, aliishukuru Airtel “Shule zetu sasa zinaweza kusoma kidijitali kwenye maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu (TET) au kupata maudhui kutoka maktaba mtandao ya Shule Direct bila bila gharama ya bando, tunawashukuru Airtel kwa kuwezesha elimu ya kidijitali kufika hadi kwa wanafunzi wetu bila gharama yoyote.”
Reviewed by Gude Media
on
June 23, 2025
Rating:


