Halmashauri ya Wilaya Igunga yampongeza Rais Dk. Samia kuimarisha Hifadhi za Taifa
Na MWANDISHI WETU, SERENGETI
MKUU wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi ameishukuru serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna ilivyoimarisha Hifadhi za Taifa jambo ambalo linawavutia watalii wengi.
Hamisi ameyasema hayo wakati alipowaongoza watumishi wa halmashauri hiyo, kufanya ziara ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wilayani Serengeti mkoani Mara.
Amesema serikali ya Rais Dk. Samia imeimarisha vivutio vya utalii hususan Mbuga ya Serengeti ambapo miundombinu imeboreshwa kwa kasi kubwa, hivyo kuvutia watalii kwa wingi kutoka ndani na nje ya nchi.
Naye Mtendaji wa Kata ya Isakamaliwa, wilayani Igunga, Misambo Kanyelele amesema wamefanikiwa kuona Nyumbu, Simba, Twiga, Viboko, Swala paa, Pundamilia, tembo, kobe, nyamera, swala Tom, chui, viboko, Mamba wakiwemo ndege aina ya Mbuni, Kanga na Kware.
Reviewed by Gude Media
on
June 28, 2025
Rating:



