Mwenyekiti wa UVCCM Dar Nasra asisitiza wavuvi na mama lisehe kushiriki Uchaguzi Mkuu, Oktoba
Na MWANDISHI WETU
Mwenyekiti wa Umoja wa Viana ( UVCCM) Mkoa wa Dar es salaam , Nasra Mohamed amesisitiza wananchi umuhimu kushiriki uchaguzi mkuu huku akiwataka kuwa chagua viongozi bora wanaotakana na CCM.
Ameyasema hayo, katika mwendelezo wa ziara yake mkoani humo, kukutana na Makundi mbalimbali ya wananchi kusikiliza na kutatua kero zao.
Aliwasisitiza kuwa hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kuzuia uchaguzi kwani ndiyo njia pekee ya kupata viongozi watakao tatua changamoto zinazowakabili.
Alieleza namna ambavyo utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi imechochea unafuu mkubwa kwa wananchi wa Tanzania hasa wananchi wa hali ya chini.
Katika ziara hiyo, inayotambulika kwa jina la OP 763 SAMIA NI SULUHU inayokusudia kuyafikia matawi 763 ya mkoa wa Dar e salaam Ndugu. Nasra ametembelea eneo la fukwe ya Minazi Mikinda lilipo mtaa wa Feri Kata ya Kigamboni na kukutana na wavuvi pamoja na mama lishe wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo.
Vilevile, Kwa pamoja wavuvi na mama lishe hao katika eneo la Minazi Mikinda wameahidi kushiriki uchaguzi ifikapo oktoba kwakuwa wanaimani kubwa na serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo amefanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM kwa zaidi ya asilimia 95.
Reviewed by Gude Media
on
June 12, 2025
Rating:

