Rais Dk. Samia: Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuwezesha malezi na upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wenye mahitaji maalumu
Na MWANDISHI WETU
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali, katika kuboresha mifumo ya kiutendaji, kiutekelezaji kuwezesha malezi na upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wenye uhitaji maalumu.
Amechangia sh. milioni 100 kufanikisha ujenzi wa kituo hicho na sh. milioni 50 kuwezesha mahitaji mbalimbali ya kituo hicho, na wasaidizi wa ofisi yake wakitoa sh. milioni 100, huku akiwapongeza kwa jitihada hizo za kusaidia jamii hususan watoto hao wenye uhitaji maalumu mfano mzuri wa kuigwa kwa unaotakiwa kufanya na dini mbalimbali.
Pia, aliwapongeza viongozi wa kanisa hilo, kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kujali jamii kupitia watoto hao wenye mahitaji maalumu, kwani ndiyo kazi njema inayotakiwa kufanywa na viongozi wa dini, ikipeleka ujumbe wa viongozi wengine wa dini waliojionesha katika mambo mengine yasiyo endana na maadili ya dini.
Rais Dk. Samia amesema hayo jijini Dar es Salaam, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu, iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kiluteli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kinachotarajiwa kujengwa mkoani Pwani Bagamoyo, kwa thamani ya sh. bilioni sita kijulikanacho kwa jina la Kituo cha Kilutheri cha Udiakonia Bagamoyo.
Alisema lengo ni kuongeza wataalamu, vitendea kazi na kuboresha miundombinu, huku akikaribisha jumuiya za kimataifa, asasi za kiraia na mshirika kuwekeza kufanikisha azima hiyo.
“Harambee hii ni kielelezo cha kanisa katika kugusa jamii kupitia watoto wenye mahitaji maalumu, ikionesha kwa dhati pendo la kristo, sawa na maandiko ya vitabu vitakatifu yasemavyo, ndiyo maana uliponijulisha niliona umuhimu wakuja mwenyewe,”alisema.
Reviewed by Gude Media
on
June 05, 2025
Rating:



