CCM chama pekee chenye imani na vijana kuandaa viongozi wa Taif
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, (UVCCM) umesema CCM ni Chama bora kinachotambua mchango mkubwa wa vijana na kuwalea katika kulitumikia taifa.
UVCCM wameyasema hayo kupitia taarifa yao, waliyoitoa ambayo imeeleza kazi kubwa ya CCM ilivyoweka misingi mizuri ya kuwaandaa viongozi kupitia nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo kuwania majimboni.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa, CCM kimekuwa kikiwapa vijana nafasi ya kushiriki, kuongoza na kunufaika moja kwa moja na utekelezaji wa sera na Ilani ya uchaguzi.
Pia, vijana wa CCM sio watazamaji, bali wamekuwa nguzo muhimu ya siasa, maendeleo na mageuzi ya kijamii kwa maendeleo endelevu ya taifa.
“Katika historia ya harakati za kisiasa nchini, vijana wamekuwa mstari wa mbele, Mwalimu Julius Nyerere alishiriki kuanzishwa TANU akiwa na miaka 32 na Mzee Rashid Kawawa akiwa na miaka 28 na uhuru wa Tanganyika umepatikana mwaka 1961 Mwalimu Nyerere akiwa na miaka 37.
“Hii ni ishara tosha kuwa msingi wa mapambano ya uhuru na maendeleo ya taifa, ulijengwa na vijana. CCM imerithi urithi huu kwa dhati na kuendeleza mtazamo huo kwa vitendo, tunaona kwa macho yetu kuwa CCM ni chama kinachowapa fursa kubwa vijana na kutambua mchango wao,”ilisema.
Katika hilo, mfano mzuri ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM katika ngazi yeyote ni mjumbe wa kikao cha kamati ya siasa, kikao cha halmashauri kuu kwa ngazi husika, hii inamaana vijana wanashiriki katika maamzu yote ndani ya jamii.
Ilisema CCM iendelea kuwa na Imani kubwa sana na vijana tumeshuhudia ziadi ya asilimia 50 vijana wameteuliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi kama wakuu wa wilya, wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa mikoa, mawaziri, wabunge, hakika kinatambua mchango wa vijana katika maendeleo ya taifa.
ANAYEWAJALI VIJANA
Chini ya uongozi wa Dk. Samia, CCM imeonyesha uthubutu na dira ya kweli kwa kizazi kipya kizazi cha vijana. Dk. Samia ameendelea kufungua milango ya ajira, elimu, uwekezaji na diplomasia inayoleta fursa mpya kwa vijana.
Baadhi ya hatua zilizotekelezwa na Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan ni Ajira kwa Vijana, ambapo zaidi ya ajira 8,084,203 zilitengenezwa kati ya 2020 hadi 2024, ambapo zaidi ya 7 milioni ni ajira zisizo rasmi.
Katika Ilani ya 2025-2030, CCM inalenga kuongeza kasi ya ajira kwa wastani wa asilimia saba ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka.
Mikopo kwa Vijana, kupitia mapato ya Halmashauri, sh. bilioni 96.3 zilitolewa kwa vijana 8,242 kati ya 2020 hadi 2024.
Reviewed by Gude Media
on
July 02, 2025
Rating:


