Diwani aliyemaliza muda wake Kabalika atia ni ubunge Jimbo la Temeke
Diwani aliyemaliza muda wake Kata ya Sandali, Christopher Kabalika, ametia nia ya kuwania ubunge jimboni la Temeke, baada ya kupata msukumo wa wananchi kutokana uzalendo wake na uchapakazi wake.
Diwani Kabalika amechukua fomu hiyo ya kutia nia ya Ubunge, huku akimshukuru Rais Dk.Samia kwa kasi yake ya maendeleo nchini ikiwemo Wilaya ya Temeke na kata yake ya Sandari.
Kabalika ameongoza Sandali kwa miaka 5 huku akichochea maendeleo makubwa katika kata hiyo, ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu, vyumba vya madarasa, vyoo na ofisi za walimu katika shule ya Sandari, Temeke ambazo ni msingi, sekondari.
Kama hiyo haitoshi, diwani huyo amekuwa karibu na wananchi kwa kutatua kero mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara na vivuko katika kata hiyo, hivyo kubadilisha mazingira na mwonekano wa kata hiyo.
Mara kwa mara amekuwa karibu na wananchi kusikiliza kero zao na kizitatua ofisini kwake na kufanya mikutano ya adhara kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Kabalika ni kiongozi mtulivu wa kisiasa asiye na Makuu katika utendaji wake, huku akishirikiana na viongozi wa Chama na Serikali kuanzia kata, Wilaya, kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kutatua kero zao.
Reviewed by Gude Media
on
July 01, 2025
Rating:
