Mahawanga atia nia ubunge viti maalumu Mkoa wa Dar es Salaam
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga, anayemaliza muda wake, ametia nia kutetea nafasi hiyo baada ya kuchukua fomu kuomba ridhaa ya kugombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mahawanga amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Asha Stambuli katika Ofisi za UWT Mkoa, pia amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuchochea maendeleo kwa Watanzania wakiwemo wanawake ambao amewasaidia kwa sehemu kubwa.
Katika ubunge wake, Mahawanga amewawakilisha vyema wanawake na makundi maalumu wakiwemo wenye ulemavu kwa kuhakikisha wanapata mikopo ya serikali isiyo na riba inayotolewa kupitia Halmashauri.
Amefanikiwa kutembelea vikundi mbalimbali vya makundi maalumu na kuviwezesha mitaji ya biashara na kujiendeleza, huku ajitambua wale wanaofanya jitihada zaidi za kujikwamua kupitia Mahawanga foundation.
Amehamasisha agenda ya nishati ya safi ya kufikia, kwani amefanikiwa kugawa mitungi ya gesi, iliyowezesha kumtua mama ndogo kichwani. Pia ametoa mchango mkubwa katuka kuhamasisha Wanawake wajasiriamali kuunda majukwaa mbalimbali kutokana na shughuli zao na kutoa elimu ya uchumi, fedha, fursa na ujasiriamali.
Reviewed by Gude Media
on
July 02, 2025
Rating:

