Hamis-Watumishi wa umma jitokezeni kupiga kura Oktoba 29, 2025
IGUNGA - TABORA
MKUU wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amewahamasisha Watumishi wa Umma kujitokeza kupiga kura ifikapo Oktoba 29,2025.
Aidha, amewataka kuwa mabalozi wa kuwahamasisha watumishi wengine zikiwemo familia zao kujitokeza kupiga kura siku hiyo ya jumatano kutimiza haki yao ya kikatiba.
Hamisi ametoa wito huo wakati akiongea na watumishi wa kata 29 kati kata 35 za wilaya hiyo katika ziara ya kusikiliza na kutatua changamoto zao.
Mbali na hayo, amewakumbusha Watumishi hao kuwa na mipango kazi katika utendaji wao.
"Ni vizuri mtumishi wa umma ukajiwekea mpango kazi kwa lengo la kufahamu nini unatakiwa ufanye kwa siku husika kwa sababu hatua hiyo inakuongezea ufanisi," amesema.
Reviewed by Gude Media
on
October 15, 2025
Rating:





