Makarani waongoza wapiga kura katika Uchaguzi Mkuu Wilaya ya Igunga wapata mafunzo
IGUNGA - TABORA
MAKARANI waongozaji wapiga kura 738 wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora wamepata mafunzo ya namna ya kuwapokea na kuwaongoza wapiga kura katika vituo vya kupigia kura Oktoba 29 mwaka huu.
Mafunzo hayo yametolewa leo Jumamosi Oktoba 25, 2025 katika kumbi mbalimbali za mikutano mjini Igunga.
Akizungumza kwa niaba ya makarani hao, Aisha Athumani amewaomba wananchi kujitokeza kupiga kura kwa sababu wao wamejipanga kutoa huduma bora na kwa wakati.
Jumla ya makarani 728 wanatarajia kutoa huduma kwa wapiga kura baada ya kuelimishwa mada mbalimbali na kujaza fomu namba 11 ikiwemo Tamko la kujitoa Uanachama na Kuapa Kiapo cha Kutunza Siri.
Makarani waongoza wapiga kura katika Uchaguzi Mkuu Wilaya ya Igunga wapata mafunzo
Reviewed by Gude Media
on
October 25, 2025
Rating:
Reviewed by Gude Media
on
October 25, 2025
Rating:





