Mbeto atoa 'pole' ACT kubakiwa na viongozi muflisi
Na Mwandishi Wetu, Pemba
Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa na uwezo mdogo wa kisiasa walionao viongozi wa ACT Wazalendo Zanzibar , tokea kilipompoteza aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho , Marehemu Maalim Seiif Sharif Hamad.
Vile vile, CCM imekitaja ACT kimepungukiwa na viongozi mahiri ,wenye uwezo mpana kisiasa ,ambapo waliobaki sasa ni wapiga porojo majukwani.
Ujumbe huo wa "pole" umetumwa toka CCM na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis aliyesema ACT kwa sasa kinaongozwa na Wanasiasa magube na makanjanja.
Mbeto alikitaja chama chochote makini cha Siasa , hutangaza sera zake , kutaja dira na sera zake ili kichaguliwe, badala yake wamebakiwa na viongozi muflisi wanaopiga bwaja na poroja majukwani .
Alisema baada ya viongozi wa ACT kushindwa kuwa wabunifu katika kuendesha siasa za kisasa, kimebaki kulitumia jina Marehemu Maalim Seif huku kikitegemea kupata ushindi wa Urais .
"ACT kimepoteza sifa baada ya kutokea kifo cha Maalim Seiif. Hivi sasa kinasubiri majaliwa baada ya kukosa matarajio .Hiyo ni shida kwa chama kutegemea uwezo mtu mmoja kukipa chama uhai wa kisiasa "Alisema
Aliongeza kusema tofauti iliopo kati ya ACT na CCM ,alisema chama chake kina hazina ya viongozi wenye upeo, uzoefu na maarifa ndio maana hata kikifanya mabadiliko ya viongozi hakipati athari zozote
Kadhalika, Mbeto aliongeza kusema kuwa ACT kimepoteza idadi kubwa ya Wanasiasa madhubuti ambao walifukuzwa CCM baadae wamekutana na adha na karaha ya mtu anayeitwa Ismail Jussa Ladhu .
Aidha , Katibu huyo Mwenezi alisema kundi la wanasiasa hodari waliotimliwa CCM mwaka 1987 miongoni mwao waliandaliwa wakiwa CCM na kukomaa kisiasa .
"Kwa Siasa za uzushi ,majungu na fitna mtaalam wake ni Jussa . ACT hakifiki popote akiendelea kuwa kiongozi. Hamad Rashid Mohamed amekorofisha na Maalim seif kwa njama za Jussa .Jussa ndiye aliyewafitini kina Mohamed Dedes na Juma Duni ili mmojawapo asigombee Urais " Alisisitiza Mbeto
Pia katibu huyo amewataka Wazanzibari kumchagua tena mgombea wa CCM, Rais Dk Hussein Ali Mwinyi ili akamilishe kazi alioianza ya kuitetea Zanzibar maendeleo .
"Msichoke kwenda na kumsikiliza Ian Smith wa Zanzibar akihubiri siasa za ubaguzi , chuki na hasama .Msikilizeni akipayuka kisha mpuuzeni ili mfanye hamsini zenu" Alisema Mbeto
Reviewed by Gude Media
on
October 08, 2025
Rating:
