Mbeto:Tutamlinda Rais Dk.Samia kwa gharama yoyote
Na Mwandishi Wetu, Pemba
Chama Cha Mapinduzi kimeahidi kitawalinda kwa gharama yoyote Marais Dk Samia Suluhu Haasan na Dk Huseein Ali Mwinyi dhidi ya
Vibaraka na Mamluki wachache wanaotishia Amani na Umoja wa Kitaifa nchini.
Pia CCM kimesema hila na njama za wakorofi wowote hazitafua dafu kwani Watanzania muda wote wako madhubuti.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo , Khamisi Mbeto Khamis ameitaja thamani ya uhuru na Umoja wa Kitaifa ulioasisiwa na Mwalimu Julius Nyerere na mwenzake Sheikh Abeid Amani Karume vitalindwa kwa nguvu zote.
Mbeto alisema Serikali za CCM hazitingishwi aidha na makundi ya Wanasiasa au Wanaharakati vinyangarika wasiojitambua kwa tamaa ya kupata fedha.
Alisema kila atakaejaribu kuchezea Amani, Utulivu na Mshikamano uliopo nchini , atakiona chamtema kuni na kilichomtoa kanga manyoya.
"Watanzania Hawajalala ,bado wako macho na makini muda wote .Hawatawatupa mkono Marais Dk Samia na Dk Mwinyi dhidi ya vitishio vya wanasiasa malaya walikubali kuupiga mnada Utu wao" Alisema Mbeto
Aidha, Katibu huyo Mwenezi alisema Wanasiasa na Wanaharakati wenye nia ya kuiweka rehani Amani ya Taifa letu , watakabiliwa na mwisho wa aibu na fedheha isiokadirika .
"Wasifikiri kwa wao kwa kununuliwa kwao na vipande vya sarafu nao wangeweza kuwanunua Watanzania . Toka sasa kila mmoja wao ajitafakari na kusalimu amri . Watanzania si malaya au waganga njaa" Alieleza
Katibu huyo Mwenezi alisema CCM kwa wakati huu kikiendelea na kampeni zake nchini , kinawataka Watanzania kutobabaishwa na propaganda za bei rahisi katika mitandao ya Kijamii badala yake wachapekazi na kuzalishamali .
"Ifikapo Oktoba 29 Mwaka huu Wananchi tokeni , nendeni mkapige kura vituoni bila longolongo .Nendeni mkatimize matakwa ya kikatiba,kiraia na kidemokrasia "Alisisitiza
Vike vile , Mbeto aliwataka watanzania kila mmoja atumie haki yake ya kuchagua bila kupoteza kura na kuwachagua wagombea wa CCM, Marais , Wabunge, Wawakilishi na Madiwani.
"Uchaguzi utafanyika. Matokeo yatatangazwa , Washindi watajulikana , maisha baada ya uchaguzi yataendelea kama kawaida " Alisema Mbeto
Reviewed by Gude Media
on
October 08, 2025
Rating:
