Selwa awataka wasimamizi wa miradi ya maendeleo kuacha kufanya kazi kwa mazoea
IGUNGA - TABORA
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amewataka Wasimamizi wakiwemo mafundi wanaojenga miradi ya maendeleo kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Selwa ametoa wito huo wakati alipofanya ziara ya siku nne kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo 18 yenye thamani ya takribani sh. 4.026 bilioni wilayani Igunga.
Amefafanua miradi minne Tarafa ya Igunga yenye thamani ya sh. 187.630 milioni, miradi nane Tarafa ya Manonga yenye thamani ya Sh. 2.806 bilioni, miradi minne Tarafa ya Igurubi yenye thamani ya sh. 730.600 milioni na miradi miwili Tarafa ya Simbo yenye thamani ya sh. 301.780 milioni inatekelezwa na serikali ya awamu ya sita.
"Ni lazima kuheshimu fedha za serikali na kujenga miundombinu hii kwa kuzingatia miongozo na BOQ, " amesisitiza.
Reviewed by Gude Media
on
October 06, 2025
Rating:




