UVCCM Igunga yamuombea kura za kishindo Dk. Samia
IGUNGA - TABORA
KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Gamalu Makona ameendelea kumuombea kura za kishindo Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan.
Gamalu ameendelea na zoezi hilo wakati alipokua na Kamati ya utekelezaji ya UVCCM Wilaya kuhamasisha makundi maaulumu ya Bodaboda, Mamalishe, Mafundi Seremala, Mawakala wa Mabasi katika kata ya Chabutwa, Ziba na Ibologero wilayani Igunga.
Aidha, ametoa elimu kwa makundi hayo namna sahihi ya kupiga kura kwa kutumia
karatasi ya mfano wa kupigia kura kwa lengo la kuhakikisha kura zitakazo pigwa haziaribiki na watie tiki au alama ya vema katika kisanduku cha mgombea wa chama hicho.
"Nawaelekeza wananchi wetu namna sahihi ya kupiga kura ndani ya kisanduku au kiboksi na niwaombe mfikishe elimu hii kwa wale waliyoko majumbani," ameomba Gamalu.
Reviewed by Gude Media
on
October 10, 2025
Rating:




