Zaidi ya wapiga kura 273,076 kupiga kura Oktoba 29, Wilaya ya Igunga-Hamis
IGUNGA - TABORA
MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Majimbo ya Igunga na Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amesema wapiga kura 273,076 wanatarajia kupiga kura ifikapo Oktoba 29, mwaka huu katika majimbo hayo.
Hamisi ameeleza hayo katika ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo katika wilaya hiyo mjini Igunga.
Kwa mujibu wa kifungu cha 69, (1) cha sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Hamisi amewaeleza wananchi waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la wapiga kura la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa uchaguzi utafanyika siku ya Jumatano Oktoba 29 mwaka huu.
Amesema vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura ndio vitatumika kupiga kura huku vikifunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni na kwa upande wa vituo vilivyoko Magereza kufunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa tisa alaasiri.
"Nitumie fursa hii kuwaomba na kuwakaribisha wananchi wote wa majimbo ya Igunga na Manonga kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29, Oktoba 2025 kwa lengo la kupiga kura," ametoa wito.
Reviewed by Gude Media
on
October 26, 2025
Rating:




