Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Igunga awataka wasimamizi wa miradi ya maendeleo kuhakikisha inakamilika kwa wakati
IGUNGA - TABORA
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amewataka Wasimamizi wa miradi ya maendeleo kuongeza bidii, umakini na kasi kwa lengo la kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliokusudiwa.
Selwa ametoa wito huo, wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa katika maeneo tofauti wilayani hapa.
"Tupambane ndugu zangu ! kwa sababu wananchi wanataka kuona matokeo ya miradi hii, hivyo tuongeze kasi huku tukizingatia thamani ya fedha na ubora," amesisitiza.
Aidha, amempongeza Mhandisi wa wilaya hiyo kwa kusimamia vema miradi hiyo huku akimuhimiza kuongeza usimamizi unaozingatia ubora ikiwemo kuokoa baadhi ya fedha.
Reviewed by Gude Media
on
November 23, 2025
Rating:




