Mbeto awapa somo muhimu Vijana EA
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi kimewataka Vijana Kanda ya Afrika Mashariki na Kati kuzipenda, kuzilinda na kuziiepusha nchi zao kutoziingiza kwenye kadhia ya mivutano na mizozo isio na ulazima wowote.
Pia chama hicho kimewahimiza Vijana hao kutofuata mkumbo wa pepo za fitna na ushawishi wenye taaswira ya nguvu ya Ukoloni na kuridhia kupoteza uhuru,utu na thamani ya kujitawala.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamis, ameeleza hayo huku akiyakemea makundi ya baadhi ya Vjana wa EA kwa kutojali maslahi ya nchi zao.
Mbeto aliitaja mivutano, mabishano na mizozio si katika njia sahihi ya kufikia utatuzi na mapatano yanayoweza kufanyika masahihisho kabla ya dhamira za wachota Mali na Rasilimali za nchi zao hawajafikia malengo yao .
Alisema vyombo vya Ulinzi na Usalama katika nchi zote duniani ,huapa kulinda mipaka , Usalama wa Mali na raia wake , hivyo si vyema kwa vyombo hivyo vikachokozwa au kuvijaribiwa
"Kazi za Vyombo vya dola zimetajwa kisheria na kikatiba za nchi zote .Hivyo si rahisi vikakwepa kutii dhamana hizo na kutojilinda lilipotokea tishio la hujuma au vurugu dhidi ya Amani ' Alisema Mbeto .
Aidha aliwaasa Vijana EA kutojiona si jukumu wenye kuyapenda, kuyalinda na kuyatetea Mataifa yao dhidi ya njama zozote kwani nje ya EA ,Vijana hao hawana mahali pa kuishi ' Alieleza
Katibu huyo Mwenezi alisema Waasisi wa Mataifa hayo wametumia nguvu nyingi , kupotezwa jasho na muda wao hadi baadhi yao kufa kwa kupigania Uhuru wa Mataifa hayo kwakuwa kazi ya kuleta uhuru haikuwa nyepesi.
"Bila Vijana kuwa na tahadhari watajikuta wakikwepa kubeba uzalendo hivyo kizazi cha sasa kinaweza kuingia katika historia isio na heshima . Kufuata mkumbo kama bendera inavyofuata upepo si fahari kwao "Alifafanua
Vile vile , Mwenezi huyo alisema wakoloni hawajawahi kuwa na nia njema na Afrika licha ya kurudi katika nchi zao , kwani mara zote huitamani Afrika na kutaka kuipangia masharti ya hovyo.
"Vijana wa Afrika Mashariki na kati amkeni na kataeni kutumiwa kwa kuzirudisha nyuma kimaendeleo nchi zenu . Babu na bibi zenu mnaowaona leo ni marafiki wema kwenu hawakutaka kuondoka kirahisi na kuiacha huru Afrika", alisema.
Reviewed by Gude Media
on
December 01, 2025
Rating:
