Igunga yaibuka kidedea kundi la mamlaka za serikali za mitaa Maonesho ya Nanenane ngazi ya kanda
TABORA
HALMASHAURI ya Wilaya ya Igunga imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Mamlaka za Serikali za Mitaa (Tabora na Kigoma) wakati wa Maonesho ya Nanenane mwaka 2025 ngazi ya kanda yaliyofanyika Uwanja wa Maonesho Ipuli - Tabora.
Aidha, imeshika nafasi ya pili katika kundi la washindi wa jumla wa mikoa ya Tabora na Kigoma wakati wa Maonesho hayo.
Akizungumza baada ya Halfa hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Ndug. Elizabeth Rwegasira amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Selwa Hamid kwa ushirikiano mzuri na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Grace Nyamwanji kwa kufanikisha ushindi huo.
Kwa ipande wa Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halamshauri hiyo, Grace Nyamwanji amewashukuru na kuwapongeza, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watumishi na Wadau wote waliyoshiriki maonesho hayo kwa sababu wao ndio chachu ya ushindi huo.
