BONANZA LA MICHEZO TRA NA WAFANYABIASHARA KATIKA VIWANJA VYA JKM PARK


NAIBU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hassan Mcha, akikabidhi kwa Nahodha wa timu ya Wafanyabiashara Kariakoo, Shafii Salimu, kombe baada ya kuifunga timu ya TRA, katika michuano ya bonanza la Siku ya mlipakodi, viwanja vya Michezo Jakaya Kikwete, Dar es Salaam, jana.




NAIBU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hassan Mcha, akikagua timu ya Wafanyabiashara Kariakoo na TRA, katika bonanza la michezo katika viwanja vya Michezo Jakaya Kikwete, Dar es Salaam, jana. Mwenye miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo. Timu hizo zilitoka suluhu.


Timu ya Wafanyabiashara Kariakoo wakishangilia baada ya kuibuka bingwa katika mpira wa miguu katika bonanza hilo.


Washiriki wa bonanza hilo wakichuana katika mchezo wa kukimbia na gunia.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, akimvisha medali mmoja wa washiriki wa bonanza la michezo la TRA na Wafanyabiashara.


Washiriki wakichuana katika mchezo wa bao.


Washiriki wakichuana katika mchezo wa karata.