Balozi Liberata Mulamula (MB), ni miongoni mwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa, watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa CCM Maalum utakaofanyika kuanzia kesho Januari 18 na19 Dodoma, kumchagua Makamu Mwenyekiti.
Akizungumza na jijini Dodoma, jana, amesema CCM iko imara, amefurahi maandalizi ya Mkutano wa Chama na yuko tayari kushiriki mkutano huo.
"Chama Cha Mapinduzi CCM), kiko imara zaidi, Ngar'i Ngar'i mambo ni moto, tunamsubili Makamu Mwenyekiti wa Chama, katika mkutano Mkuu wa kesho," amesema.