CCM Tanga, yaahidi kura za kishindo kwa Rais Dk.Samia Uchaguzi Mkuu 2025
Na MWANDISHI WETU
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga , Rajab Abdallah, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, amemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya ziara mkoani humo na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo, jambo linalowaachia deni kubwa ya kumpatia kura za kishindo 2025.
Abdallah ameyasema hayo mkoani humo wakati Rais Dk.Samia akiwa katika Jimbo la Pangani ambako alipokelewa na mamia ya wananchi wa Wilaya hiyo na Tanga kwa ujumla.
"Mafanikio yote yanatokana na kibali cha Rais Dk.Samia, wanatanga tumeshaamua, kwenda na Rais Dk.Samia katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu, kuhakikisha Mkoa wa Tanga unaongoza kwa kukupatia kura nyingi na wameagiza wenyeviti wa CCM kuhakikisha tunatafuta kura za kishindo wakati ukifika" alisema
Alisema mapokezi mazuri ya wanatanga katika mikutano ya Rais Dk Samia mkoani humo, ni upendo wao kwa kiongozi huyo wa nchi kwa kushuhudia ziara hiyo katika maeneo mbalimbal ya Kata ya Tanga, kufungua miradi na kutatatua changamoto mbalimbali ikiwemo barabara.
"Wapinzani, hawana hoja Tanga kwani Rais Dk.Samia ametoa fedha nyingi za utekelezaji Ilani kwa miundombinu mbalimbali, kwani hoja zao za kielimu hazina mashiko, maana viongozi mbalimbali wa Mkoa huo wamesoma shule za kata na kufanikiwa kielimu, wameendelea kutoa fedha za kujenga vyumba vya madarasa, kutoa fedha za kununua madawati kuhakikisha hakuna mwananchi anaye kaa chini," alisema.
CCM Tanga, yaahidi kura za kishindo kwa Rais Dk.Samia Uchaguzi Mkuu 2025
Reviewed by Gude Media
on
February 26, 2025
Rating:
