Lengo la warsha lilikuwa kuwafundisha wazazi kuwa sehemu ya mchakato wa kufanyiwa mazoezi ya lugha watoto wao baada ya kuanza kusikia kupitia vifaa vyao vya usikivu.
Wazazi 60 walinufaika na warsha hii iliyofanywa na wataalam wa ndani kutoka Kliniki ya HearWell ambao walifundishwa na MEDEL katika mtaala huu maalumu.
Fayaz Jaffer, mratibu wa warsha huu na mtaalamu wa usikivu kutoka Kliniki ya HearWell alisema, “Tunashukuru MEDEL kwa mpango huu muhimu unaohusisha wazazi na walezi kwa kuwapa mafunzo kuwa sehemu ya mchakato wa maendeleo ya lugha za watoto wao."
"Hii ni warsha ya kwanza ya aina hii iliyowasilishwa kwa lugha ya KISWAHILI, na kulingana na jinsi itakavyopokelewa na wazazi, tutakuwa na warsha kama hizi mara kwa mara," aliongeza.
"Wazazi wanapaswa kuangalia ishara zozote za ucheleweshaji wa hatua za lugha na kutafuta msaada wa kitaalamu ikiwa wana shaka," alisema Bi. Rashida Hassuji ambaye ni Mtaalamu Mkuu wa Sauti na Lugha katika kliniki ya HearWell.
“Kwa kuwa tuna zana za kisasa za uchunguzi na wataalamu wa ndani katika fani huu, mtu hahitaji kusafiri nje ya nchi tena kwa ajili ya tathmini. Ikiwa inahitajika, vifaa vya kisasa vya kusikia vinapatikana hapa nchini na upasuaji wa Cochlear Implant pia unafanywa nchini siku hizi na wataalam wetu" aliongeza.
Wazazi walioshiriki walipongeza timu ya HearWell kwa jitihada zao zote katika kuandaa warsha hii. Walithamini kila walichojifunza wakati wa warsha na kwamba itawasaidia kushiriki katika safari ya maendeleo ya lugha ya watoto wao.