AIRTEL yaunga mkono TCRA kubaini Utapeli unaofanyika kupitia SMS
Akieleza hilo, Meneja Mahusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema kwa kutumia Akili Mnemba, Airtel imetumia kuwajulisha wateja wake kubaini matapeli wanaojaribu kufanya njama za kuwadanga wateja kupitia ujumbe mfupi au meseji zinazotumwa na waarifu.
Alisema huduma hiyo niya kwanza kwa mitandao ya simu iliyopo nchini kulinda wateja wake, ambayo inatumika pasipo kuwa na gharama zozote kwa wateja wa Airtel.
“Kupitia huduma hii, tunaunga mkono Mamlaka ya Mawasiliano TCRA ya stapeliki, inayolinda watenja dhidi ya vikundi vya utapeli nchini vinavyofanywa kupitia mitandao ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi ikiwemo Tuma kwa namba hii hivyo kwa hatua hiyo mteja ataweza kugundua na kuepuka utapeli huo,”alisema
Alisema kuwa wanayo huduma nyingine ya kadi ambayo inawasaidia wateja wao kuweka fedha katika kadi hiyo kuwawezesha kununua bidhaa mbalimbali kwa muda wowote na wakati wowote.
Alisema kuwa katika msimu huu wa SABASABA wanazoofa kubwa za vifurushi vya mawasiliano na simu zenye unafuu mkubwa.
