RC Chacha ameahidi kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu
Na MWANDISHI WETU
UYUI - TABORA
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amemuahidi Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025, Ismail Ussi kuendelea kuwahamasisha wananchi washiriki uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Chacha ametoa wito huo wakati wa mapokezi na makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru 2025 yaliofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Tura wilayani Uyui mkoani hapa.
Amedokeza Mwenge wa Uhuru unatembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo 57 yenye thamani ya sh. 38.8 bilioni.
Kwa upande wa Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025, Ismail Ussi aliahidi kulinda heshima ya wananchi wa mkoa huo huku akiwashukuru na kuwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi na makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru.
