DC Sauda awataka Mgambo waliohitimu mafunzo kuwa waadilifu na wazalendo kwa Taifa
Na MWANDISHI WETU
MKUU wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Sauda Mtondoo amewaasa askari wa Jeshi la Akiba ambao wamehitimu mafunzo yao kuendelea kuwa waadilifu na wazalendo kwa Taifa lao.
Sauda ametoa wito huo, wakati akifunga mafunzo hayo yaliyodumu kwa miezi mine katika kijiji cha Mwanzugi wilayani hapa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mshauri wa Jeshi la Akiba wa wilaya hiyo, Meja Ayadi Amiri amesema askari waliohitimu ni 102 ambapo wanaume ni 84 na wanawake ni 18.
Kwa upande wa wahimu hao, MG. Charles Taungiru amesema mafunzo waliyoyapata yamewajengea uzalendo, uadilifu, uaminifu, uvumilivu, ukakamavu na kuwawezesha kufahamu nia na moyo wa kulinda Taifa lao.
DC Sauda awataka Mgambo waliohitimu mafunzo kuwa waadilifu na wazalendo kwa Taifa
Reviewed by Gude Media
on
August 28, 2025
Rating:
