Mkurugenzi Halmashauri Wilaya Igunga Selwa, amshukuru Rais Dk. Samia kuwaongezea bajeti ya ushiriki wa timu ya watumishi katika michezo ya SHIMISEMITA
IGUNGA - TABORA
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amemshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaongezea bajeti jambo ambalo limesaidia yeye kuiwezesha timu ya Watumishi wa Halmashauri kushiriki michezo ya SHIMISEMITA jijini Tanga.
Selwa ametoa pongezi hizo wakati akiwaaga watumishi wanaokwenda kushiriki michezo iliyoandaliwa na Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA).
Amesema ni wajibu kuendelea kumshukuru Rais Dk. Samia kwa kuwawezesha bajeti iliyofanikisha jambo hilo ambalo limeandika historia ya Halmashauri hiyo kushiriki kwa mara yakwanza tangu ilipoanzishwa 1994.
’Ninafurahi mtakavyopeperusha bendera ya Igunga huko jijini Tanga, jambo la msingi ni kushiriki vema hivyo jisikieni fahari na mkacheze kwa bidii, nidhamu na heshima,’’ amesema.
