Halmashauri ya Wilaya ya Igunga wapongezwa kliniki ya ardhi
IGUNGA - TABORA
OFISA Maendeleo ya Ardhi wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Jusper Tito amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Selwa Hamid kwa kufanikisha Halmashauri kupata hati miliki yake.
Jasper ametoa pongezi hizo wakati wa kliniki ya ardhi na ugawaji wa Hati Miliki kwa wananchi wa Kijiji cha Igurubi wilayani hapa.
"’Jukumu letu baada ya urasimishaji makazi ni kuwafuata Wananchi kuwapa huduma mahali walipo kwa sababu kutoka Igurubi hadi Igunga kunakilometa 52, hivyo kumsumbua mwananchi kusafiri umbali mrefu sio vizuri,’’ amesema.
Naye Msajili Msaidizi wa Hati wa mkoa huo, Emily Masoga amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuipendelea Wizara ya Ardhi kwa sababu ameipatia vifaa vya kutosha na miradi mikubwa.
