PUGU WAVUNJA MAKUNDI YA UDIWANI
HATIMAYE makundi ya watia nia udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Pugu wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam yamevunjwa rasmi kwa watia nia ambao kura za maoni hazikutosha kumuunga mkono mgombea Udiwani wa kata hiyo Frank Mang'ati.
Mkutano Chama wa kuvunja makundi hayo umefanyika leo ambapo ulihudhuriwa na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela, ambaye katika uchaguzi wa ndani wa CCM kura zake hazikutosha.
Aliyekuwa mtia nia mwingine ambaye alihudhuria kikao hicho ni Magere Paul ambapo kwa pamoja walikubaliana kumuunga mkono Mang'ati na kuhakikisha CCM inashinda katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Katika hotuba yake, Mgombea Udiwani wa Kata ya Pugu, Mang'ati, amesema ni wakati wa Wana CCM katika kata hiyo kushikamana kuhakikisha anashinda.
PUGU WAVUNJA MAKUNDI YA UDIWANI
Reviewed by Gude Media
on
August 17, 2025
Rating:
