Wasimamizi wasaidizi ngazi kata wapewa mafunzo
IGUNGA - TABORA
MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Igunga na Manonga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi ameendelea kukagua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya kata kwa lengo la kuhakikisha watasimamia vema taratibu za uchaguzi mkuu katika maeneo yao.
Hamisi amefanya ukaguzi huo wakati mafunzo hayo ya Uchaguzi ambayo yanaingia siku ya pili yanayofanyika kwa wasimamizi hao katika ukumbi wa Maxwel mjini hapa.
Aidha, amewataka Wasimamizi hao kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi muda wote wa utendaji wa majukumu yao.
Amesema hatua hiyo itaweupesha na makosa ya kila aina wakati wa zoezi hilo, hivyo watahakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi, amani na utulivu chini ya kauli mbiu isemayo:" Kura Yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura".
