Halmashauri ya Igunga yampongeza Rais Dk. Samia
IGUNGA - TABORA
MKUU wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amemshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza mishahara na kupandisha watumishi vyeo.
Hamisi ametoa shukrani na pongezi hizo wakati akiongea na watumishi 300 kutoka katika Kata sita katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa Bishop Batenzi Hospitali ya Rufaa Nkinga Kata ya Nkinga mjini hapa.
Amesema serikali inawapenda watumishi kwa sababu imefanya kila namna kuwapandisha vyeo.
Kwa upande wa Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TAGLU) wa mkoa huo, Ali Nguli amewaeleza watumushi hao kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) upo, hivyo wanapopata majanga mahala pakazi wautumie mfuko huo.
