Miundombinu iliyojengwa na serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia yaongeza ufaulu kwa wanafunzi kidato cha sita Wilaya ya Igunga-Selwa
IGUNGA - TABORA
MIUNDOMBINU iliyojengwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetajwa chachu ya ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha sita kwa aslimia 100 kwa shule za wilaya ya Igunga mkaoni Tabora.
Akizungumza na Walimu wa Shule za Seondari Igunga, Nanga, Ziba, Mwisi na Choma ambazo nì za kidato cha tano na sita wakati wa hafla yakuwagawia Sh. 5 milioni kwa ufaulu huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Selwa Hamid amesma Rais Dk. Samia amefanya kazi kubwa.
Ameeleza amejenga miundombinu, kuongeza ajira za walimu na kuongeza mishahara kulikofanywa na Rais Dk. Samia ni sababu inayochagiza ufaulu huo.
Amefafanua Wanafunzi 1045 walifaulu kwa asilimia 100 ambapo wanafunzi 839 walipata daraja la kwanza, wanafunzi 200 walipata daraja lapili huku wanafunzi wanne wakipata daraja la tatu na hakukuwa na daraja lanne au zero.
"Tunapaswa tujipongeze ndugu zangu Walimu, hakika hii ni heshima kubwa kwa wilaya, mkoa na Taifa kwa shule ya kata kuingia kumi bora, tunatembea kifua mbele," amepongeza.
