Walimu wa IT Zanzibar wapewa ujuzi wa smart wasomi wa Airtel
KAMPUNI ya Mawasilino ya Airtel Tanzania, kupitia Airtel Africa Foundation kushirikiana na Shirika la kimataifa la Watoto (UNICEF) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imeendesha warsha ya mafunzo kwa walimu wa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Airtel SmartWASOMI.
Akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari Zanzibar, Asia Iddy Issa, alisifu mpango huo unaokwenda sambamba na malengo ya kitaifa.
Alisema Mpango huo wa elimu ya kidijitali unalenga kuongeza upatikanaji wa elimu bora kupitia teknolojia kote nchini Tanzania ukiwaunganisha walimu 36 kutoka shule mbalimbali za sekondari ambazo tayari zimeunganishwa na jukwaa la Airtel SmartWASOMI visiwani Zanzibar.
“Mpango huu unasaidia ndoto yetu ya kuunda kizazi chenye uelewa wa kidijitali na unatatua changamoto zilizokwamisha upatikanaji wa nyenzo bora za kujifunzia, hasa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa kwa kuwajengea uwezo walimu na kuondoa kikwazo cha gharama za data, tunapunguza pengo kati ya mbinu za kiasili za ufundishaji na ufundishaji wa kisasa,” alisema Asia
Tangu uzinduzi Smart WASOMI mwezi Mei mwaka jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mpango huo umefikia zaidi ya shule 400 na umeleta athari chanya kwa maelfu ya walimu na wanafunzi nchini.
