Na MWANDISHI WETU
Mlezi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata za Makongo, Kinondoni na Bunju, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam ambaye ni Diwani wa Viti Maaumu, Grace Mwashala, amekabidhi msaada wa wa vitu mbalimbali vyenye thamani y ash. 1,200,000 kwa uongozi wa UWT Kata ya Kinondoni, jijinii Dar es Salaam.
Diwani huyo amekabidhi vitenge 55,kadi za UWT 333 , fedha ya kufungua akauti 20,000 na fedha za kuanzia akiba katika akaunti sh. 50,000.
Grace amesema dhamira ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwakwamua wanawake kiuchumi kwani vitu hivyo alivyo kabidhi ni kwaajili ya kuanzisha mradi ambapo fedha itakayopatikana itaingizwa katika akauti ya UWT ya kata hiyo.