Vikundi 88 vimepatiwa mkopo wa bilioni 1. 2 Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
IGUNGA - TABORA
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, John Tesha amesema serikali inaendelea kuwatendea haki wananchi wake kwa sababu wanakikundi 408 kutoka kwenye vikundi 88 wamenufaishwa na sh. 1.2 bilioni.
Tasha ameyaeleza hayo wakati wa Hafla ya kukabidhi hundi kwa vikundi vilivyokidhi vigezo kupata mkopo iliyofanyika katika ukumibi wa Halmashauri hiyo mjini Igunga.
Aidha, ameikumbusha jamii kuwa utoaji wa mikopo hiyo ni endelevu huku akiwasisitiza waliokopeshwa kutekeleza miradi waliyoombea fedha na siyo vinginevyo.
"Hakika tunaendelea kuishukuru serikali ya Awamu ya Sita ambayo imeendelea kuajiri Maofisa Maendeleo ya Jamii ambao wanaendelea kutoa elimu kwa wanachi kuhusu namna bora ya kupata mikopo hii ambayo mchakato wake unaanzia ngazi ya kata," amesema.
Reviewed by Gude Media
on
December 03, 2025
Rating:



