TWIGA STARS YAFUZU RAUINDI YA PILI WAFCON

 Timu ya taifa ya Wanawake Twiga Stars,  imefuzu raundi ya pili ya Michuano ya Afrika ya Wanawake WAFCON, baada ya kuifunga timu ya taifa ya wanawake ya Ivory Coast, kwa mikwaju ya penati 4-2.


Mchezo wa kwanza ulichezwa nchini Ivory Coast, Twiga Stars ilipoteza kwa mabao 2-0, ambapo leo ulikuwa mchezo wa marudiano Twiga Stars imefanikiwa kuifunga timu hiyo mabao 2-0, na matokeo kuwa mabao 2-2.