TAWA KUIBADILI KILWA KUWA MJI WA KITALII

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai




NA WILLIAM KAPAWAGA, KILWA


MAMLAKA ya Usimamizi wa wanyamapoli Tanzania (TAWA), Wilayani Kilwa imejipanga kubadili mji huo wa kale kuwa moja ya miji ya Kitalii hapa nchini.


Hiyo inatokana na mipango na uwezeshwaji unaofanywa na serikali  kupitia wizara ya Maliasiri na Utalii  katika wilaya hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher  Ngubiagai, amesema huo ndiyo mkaati wa ofisi ya wilaya pamoja na TAWA.


Ngubiagai amesema TAWA inajukumu kubwa katika mji huo kutokana ma kuwa na vivutio na hustoria kubwa kwa nchi na dunia kwa ujumla.


Amesema kutokana malikale na vituo mbalimbali vya Kilwa huo ulitakiwa kuwa mji wa kisasa zaidi na wenye kuvutia watalii wengi na wageni mbalimbali.


Kutokana na mikakati ya TAWA wilayani Kilwa na maekekezo na uwezeshaji unaofanywa  ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ana amini kuna mabadiliko makubwa yatatokea ndani ya Kilwa 


Ametoa mfani mfano wa Kilwa Kisiwani na Songo Mnara yalikuwa majiji ya Kiswahili ya kibiashara na ustawi wake ulitegemea umilikaji wa Biashara na Bahari ya Hindi.


Ngubiagai amesema kutokana na  hilo  ilizifanya nchi za Uarabuni, India na China hasa katika karne ya 13 hadi 16 kufanya kama kituo cha biashara 


"Mji wa Kilwa Kisiwani ulikiwa mji pekee katika Pwani ya Afrika Mashariki kutengeza na kutumia sarafu yake katika karne ya 11", amesema.


Aidha amesema TAWA inajipanga kuhakikisha kutangaza eneo hilo kutokana na vivutito vya Msikiti Mkuu mkongwe katika Pwani ya Afrika Mashariki 


Kwa upande wa Songo Mnara, Ngubiagai amesema kuna vivutio kama magofu ya misikiti na na nyumba za makazi ya watu wa kale.


Baada ya kukabidhiwa usimamizi wa hifadhi ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara TAWA imefanya maboresho ya miundombinu ya Utalii ili kuvutia watalii.


"Kufuatia marekebisho yaliyofantika katika eneo la Kilwa Kilwa Kisiwani na Songo Mnara idadi ya watalii imeongezeka kutoka 2,988 mwaka  2018/19:hadi 6,370 mwaka 2022/24", amesema.


Amesema hiyo ni juhudi na mikakati mikubwa inafofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi imara wa Rais Samia Suluhu Hasdani.