Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Arusha wakiwa katika matembezi ya kuliombea Taifa, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika, leo Desemba 9, 2024.
Matembezi hayo yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwa kushirikiana na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani humo.
Maombi maalumu ya kuliombea Taifa yamefanyika katika Viwanja vya pembezoni mwa mzunguko wa barabara katika Mnara wa Mwenge ijini Arusha.