KIONGOSI - SIMIYU INAUNGA MKONO AZIMIO LA CCM, RC WANAOTAKA URAIS NDANI YA CCM JAMBO LIMEKWISHA.

Na MWANDISHI WETU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi, ameshiriki katika matembezi ya kuunga mkono azimio la Chama cha Mapinduzi (CCM) ambalo limemteua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.

Akizungumza baada ya matembezi hayo yaliyofanyika Mjini Bariadi, Kihongosi amesema  Simiyu wanaunga mkono azimio hilo lililompitisha Dk. Samia na mgombea mwenza wake Dk.Emanuel Nchimbi ili wakaendelee na kazi walioianza.

Kihongosi amesema, maendeleo yaliyopatikana sasa hayafanani na yale ya miaka minne iliyopita ikiwemo ukamilishwaji wa mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere unaogharimu Trilioini 6.5.

“Kabla Rais Samia hajaingia madarakani reli ya kisasa ya SGR inayogharimu tril 7.2 ilikuwa haijakamilika na sasa imeanza kazi kwa kipoande cha Dar es Salaam hadi Dodoma, huko mkoani Mwanza ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi maarufu Daraja la Magufuli unaogharimu Bil 700 umefikia asilimia 96,” amesema.

Pia Kihongosi amesema hakuna sababu za MwanaCCM yeyote kuogopa wala kuhofia kwa sababu utekelezaji wa Ilani ya umekamilika kwa asilimia kubwa ikiwemo ujenzi wa Shule ya Wasichana Bariadi Kusini, kujengwa kwa shule ya Wavulana Simiyu Boys, na kwa kuwa mkutano mkuu umeshaamua mtu yeyote mwenye nia ya kuwania urais shughuli imeisha na atakayemtweza Dk. Samia, CCM itashughulika naye.