MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini, (LATRA), imesema itaendelea kudhibiti ajali kwa kuweka vituo vya ufuatiliaji wa magari katika maeneo ambayo madereva wa mabasi ya usafirishaji abiria wanayatumia kufanya udanganyifu kuepusha suala hilo
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy wakati akizungumzia kazi kubwa iliyofanywa ya udhibiti wa usafiri kipindi cha siku kuu za mwisho wa mwaka.
Amesema hali ya Udhibiti wa ajali nchini imeimarika na huduma zimeendelea kuboreshwa huku madereva wakiongeza umakini kwasababu ya mfumo mzuri wa ufuatiliaji uliopo wa VTS, ambapo dereva anatambuliwa hadi jina lake.
Amesema hali ya usafirishaji wa abiria kipindi cha sikukuu za mwaka ilienda vizuri na udhibiti ulifanyika vizuri kuwawezesha wasafiri kupata huduma bora.
Pazzy amesema katika kipindi hicho abiria wanao tumia usafiri wa mabasi na treni, walisafiri vyema pasipo na usumbufu wowote hivyo kuwawezesha kufika salama kwa wepesi kutoka na uimara wa usafiri huo.
Amesema katika hicho cha siku kuu, ajali kubwa zilikuwa sita na iliyohusisha basi ni moja, kutokana na kazi kubwa ya udhibiti iliyofanyika.