LATRA YASISITIZA USAJIRI WA SPECIAL HIRE KWENYE MFUMO WA VTS

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imewataka madereva na wamiliki wa mabasi maalumu ya kukodi (special Hire), kufika ofisi za LATRA kusajiliwa na kuunganishwa katika Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS)kabla ya Januari 12 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy, amesema kwa mujibu wa kanuni magari hayo yatakiwa kusajiliwa kwa VTS.

"Kwa mujibu wa kanuni ya 20(b) ya Kanuni za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za magari ya kukodi za mwaka 2020, mabasi hayo ya (Special Hire)yanapaswa kuunganishwa na Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS). 

"Mfumo huo huwezesha Mamlaka kuyatambua dereva anayeendesha gari husika endapo dereva huyo atasajiliwa na kutumia Kitufe cha Utambuziwa Dereva (i-button)", amesema.

Amesema kanuni ya 9(2) ya Kanuni za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Uthibitishaji Madereva, yanayopaswa kutumia Kitufe cha Utambuzi wa Derevaambapo Mabasi Maalumu ya kukodini na usajili wahudumu wa vyombo vya moto kibiashara mamlaka ina jukumu la kuainisha magari miongoni mwa magari yaliyo ainishwa.