WATUMIAJI BAHARI YA HINDI WACHUKUE TAHADHALI KIMBUNGA DIKELEDI

Na MWANDISHI WETU 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wananchi hususan watumiaji wa Bahari ya Hindi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka hiyo na kuchukua tahadhari kufua taarifa ya uwepo wa kimbunga “DIKELEDI” katika Bahari ya hiyo mwambao wa Pwani ya Msumbiji.

Taarifa hiyo imetolewa na TMA, jana, imesemamifumo ya hali ya hewa inaonesha kimbunga hicho kwa sasa kipo katika mwambao wa Pwani ya Msumbiji na kinatarajiwa kurejea katika Rasi ya Msumbiji.

"Watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta,"amesema taarifa.

 Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kimbunga hicho hakiashirii uwezekano wa kusababisha athari za moja kwa moja hapa nchini. Hata hivyo, kutokana na ukaribu wa maeneo ambayo kimbunga “DIKELEDI” kipo sambamba na maeneo ya kusini mwa nchi yetu.