Na MWANDISHI WETU
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema jitihada kubwa za uwekezaji zilizofanywa na serikali katika kilimo cha kahawa, zimesaidia kuongeza uzalishaji nchini na kuchochea ukuaji uchumi wa wakulima wa zao hilo na serikali.
Bashe ameyasemayo jijini Dar es Salaam, , alipokuwa akifungua mkutano wa tatu wa Kahawa kwa nchi za Afrika (The 3rd G25 African Coffee Summit 2025), uliowakutanisha Mawaziri wa Kilimo wa nchi 25 za Afrika na viongozi wa Taasisi mbalimbali za kilimo cha kahawa.
Mkutano huo wenye kauli mbiu ya "kufungua ajira kwa vijana kupitia uendelezaji wa sekta ya kahawa Afrika" unalenga kujadili mustakabali wa maendeleo ya zao la kahawa Afrika.
" Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha inainua zao kahawa. jitihada hizo ni kuzipa nguvu Taasisi za utafiti na kupambana magonjwa ya kahawa, kuanzisha mpanga wa kuendeleza vijana na wanawake katika kilimo ikiwemo kahawa, (BBT) ili kuchochea ulaji, kuwekeza katika viwanja vya usindikaji ikiwemo TANICA, kutoa pembejeo ikiwemo mbegu na mashine za kisasa kwa wakulima," amesema.
Amesema mikakati hiyo imesaidia Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji wa kahawa, huku jitihada zaidi ziliendelea kufanywa na serikali kuhakikisha inaongeza hamasa zaidi kwa vijana na wanawake kujikita katika kilimo cha kahawa, kuongeza uzalishaji zaidi ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kufikia mageuzi makubwa ifikapo 2030.
Bashe, amesema kwa jitihada hizo zimesaidia kufikia mafanikio makubwa ya uzalishaji kutoka asilimia saba kufika 15 huku uzalishaji ukiongezeka zaidi kwasasa ikitokana na hamasa kubwa waliyoifanya nchini ya kutambulisha mpango mauzo ya soko kwa ngazi vijiji hususan Mkoa wa Kagera ikijulika kama KIOSKI, ambayo imekuwa chachu kubwa ya uzalishaji.