Na MWANDISHI WETU
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi, ameendelea na ziara yake ya kikazi ya kutatua na kusikikiza changamoto za wananchi katika mkoa huo.
Kiongosi amesema wananchi wazidi kufanya kazi na kushirikiana na serikali, pia amesema Rais Dk Samia Suluhu Hassan alipomteua alimuagiza asimamie haki za wananchi pamoja na kusimamia fedha za miradi ya maendeleo.
Kihongosi amesema hayo alipokuwa anazungumza na wananchi katika Machimbo ya Ikinabushu na kupokelewa na Maelfu ya Wananchi.
Amewasisitiza wananchi wa mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa bidii kukuza uchumi wao, Taifa na kumuombea afya njema Rais Dk Samia katika utekelezaji wa majukumu yake.